Ismail Mgunda ajiunga AS Vita
Hatimaye Ismail Mgunda wa Mashujaa FC ya mkoani Kigoma amekamilisha dili la kujiunga na timu ya AS Vita Club ya DR Congo.
Mchezaji huyo tayari amejiunga na timu hiyo na ameanza mazoezi akijiandaa kuitumikia timu hiyo katika michuano mbalimbali.
Mgunda ni chaguo la kocha wa timu hiyo Youssuph Dabo raia wa Senegal ambaye alimuona wakati akiinoa Azam FC.