Haji Manara asisitiza Yanga itachukua ubingwa hadi 2030
Mwanachama na Shabiki wa Yanga,Haji Manara amesema ahadi yake juu ya Klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa NBCPL hadi 2030 ipo pale pale lakini iwapo watapoteza basi sababu kuu itakua ni kutokana na kukosekana kwa umoja ndani ya kikosi chao.
.
"Iwapo tutapoteza Ubingwa basi sababu ni kukosekana kwa umoja wa asilimia miamoja,mara zote Yanga ilipopoteza Ubingwa miaka yote ilitokana na mpasuko wa ndani ambao kwa sasa haupo.
Kwa sasa umoja ndani ya Klabu ni mkubwa tena wa asilimia 100.Hata nilipokua Simba ilibidi nitumwe kuzua taharuki ili kuwaondolea utulivu"Haji Manara kupitia Clouds FM.