Cristiano Ronaldo anunua ndege kwa bil 187
Nyota wa soka, Cristiano Ronaldo, amenunua ndege mpya ya kibinafsi yenye thamani ya $75 milioni sawa na Tsh Bilioni 187.6, ikimuwezesha kusafiri kwa staili ya kipekee anapokuwa nje ya Mashariki ya Kati.
Ndege hiyo, Gulfstream G650, ina uwezo wa kufikia kasi ya 610mph na inaweza kubeba abiria 19, ikionyesha kiwango cha juu cha maisha anachoishi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39.
Ronaldo, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or mara tano, ameamua kuboresha usafiri wake baada ya kuachana na ndege yake ya awali, Gulfstream G200, yenye thamani ya $24 milioni sawa na Tsh Bilioni 60.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka chombo cha habari cha Uturuki, Daily Sabah, mchezaji huyu wa Al-Nassr, anayeshiriki katika ligi ya Saudi Pro League, sasa anamiliki ndege hii mpya ambayo inajulikana kwa uwezo wake wa kasi na yakifahari.
Ndege hiyo ya kisasa inauwezo wa kubeba hadi abiria 19, kumaanisha kwamba mpenzi wa Ronaldo Georgina Rodriguez na watoto wao wanaweza kuungana naye katika safari zake. Pia Kuna nafasi kwa wasafiri 10 walio kwenye Ndege kulala.
Ndege hii ya kisasa inamuwezesha Ronaldo kusafiri kwa urahisi, huku ikionyesha mafanikio yake makubwa katika ulimwengu wa soka. Hii ni hatua nyingine katika maisha ya kifahari ya mchezaji huyu, ambaye amekuwa akishika vichwa vya habari kwa ufanisi wake uwanjani na maisha yake binafsi.