Baleke aing' ang' ania Yanga mpaka alipwe chake
Mchezaji wa Klabu ya Yanga Jean Othos Baleke amegoma kwenda kwa mkopo katika klabu ya Namungo Fc na anataka kulipwa chake aondoke Yanga.
Yanga hawana mpango na nyota huyo wa kimataifa wa DR Congo na kinachokwamisha kuvunja mkataba wake ni baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye mkataba wake.
Ikumbukwe, baleke ameendelea kukosa nafasi ya kucheza kwenye kikosi hicho Cha yanga. Tangu wakati wa kocha Gamondi hadi sasa kwa mtaalam wa gusa achia twende kwao.