Ateba aipeleka Simba robo fainali kombe la Shirikisho
Wakubwa ni wakubwa tu naweza kutamka hivyo, wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika, Simba SC usiku huu imetinga robo fainali baada ya kuilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Bravos de Maquiz ya Angola.
Mchezo huo wa marudiano uliopigwa Angola, Simba wamefuzu robo fainali kwa Sheria ya nani aliyemfunga mwenzake, kwani Simba iliwahi kuifunga 1-0 Bravos jijini Dar es Salaam.
Bravos walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza kupitia Abedinego Mosiatlhaga dakika ya 12 kabla ya Lionel Ateba dakika ya 62 kuisawazishia Simba na kuipeleka robo fainali kwa mara ya pili tangu ilipofanya hivyo.
Kwa matokeo hayo imefikisha pointi 10 ikiwa nafasi ya pili lakini hata ikitokea imefungwa halafu Bravos kashinda idadi kubwa ya mabao haitaweza kuivuka Simba.
Hongera Simba SC