Ahmed Ally awataka mashabiki Simba kutokanyaga kwa Mkapa

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema ni vyema Wanasimba wakatekeleza adhabu waliyopewa kutoka CAF ili kuepuka madhara makubwa zaidi.
-
”Niwambie Wanasimba tuheshimu hii adhabu, mtu yoyote hata kama ni mjanja kiasi gani wa kuingia uwanjani, niwaombe Wanasimba kukaa mbali na Uwanja wa Mkapa kuna watu ambao watakuwa wanaangalia kama tumefata utaratibu.”
-
“Tuna kazi kubwa ya kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi letu. kama mnavyojua mchezo wetu tumezuiliwa kuingiza mashabiki kuingia uwanjani. Limekuwa tukio la kuumiza sana na wengine mpaka sasa bado hawajaamini, imetuchanganya pakubwa.”

“Adhabu hii ni mechi moja ambapo tukitumikia adhabu hii vizuri mechi ya robo fainali mashabiki wataingia uwanjani.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA