Yanga yakimbilia kwa Mungu
#MICHEZO: Rais wa klabu wa Yanga Hersi Said amesema anajua umuhimu wa kupata ushindi kwenye mchezo wao wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe mchezo utakaochezwa jumamosi hii, disemba 14, 2024.
"Tumuombe Mungu twende salama tukaipiganie timu yetu najua ni muhimu kupata matokeo katika mchezo huu, viongozi wanakwenda pamoja na wachezaji, benchi la ufundi ili kuipigania timu yetu na kutafuta matokeo, ikimpendeza Mungu basi turudi na alama tatu."- Eng. Hersi Rais Yanga SC.
Ilikujiweka kwenye eneo salama Yanga wanahitaji ushindi kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe Utakaochezwa Lubumbashi nchini Kongo (DRC) hadi sasa Yanga wapo mkiani kwenye msimami wa kundi A’, hawana alama hata moja baada ya kufungwa michezo yote miwili waliyocheza. Al Hilal ndio kinara wa kundi alama 6, Mc Alger nafasi ya pili wana alama 4 na Mazembe wana alama 1 nafasi ya tatu.