Yanga yaishika TP Mazembe
Mabingwa wa soka Tanzania bara Dar Young Africans jioni ya leo imeishika vibaya TP Mazembe na kuilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika uwanja wa TP Mazembe Stadium, mjini Lubumbashi, DR Congo.
TP Mazembe walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Cheick Fofana dakika ya 40, Yanga walisawazisha kupitia Prince Dube dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo Yanga itaendelea kushika mkia ikiwa na pointi 1 wakati Mazembe pointi 2.
.