Yanga warejea na bonge la rekodi
Kikosi cha timu ya Yanga SC kinewasili salama kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, (DRC) ambapo jana kilicheza na TP Mazembe na kwenda nayo sare ya 1-1 mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika.
Mchezo wa jana ndio ulikuwa wa kwanza kwa Yanga kupata pointi baada ya mechi mbili mfululizo kupoteza kwa mabao mawili bila majibu.
Taarifa nzuri kwa Yanga kwamba imekuwa klabu pekee hapa nchini kurudi na pointi nje ya nchi msimu huu, watani zao Simba SC waliambulia patupu nje ya nchi wakifungwa mabao 2-1 na CS Constantine ya Algeria.
Mechi zilizobaki kwa Yanga zitachezwa jijini Dar es Salaam hivyo Simba pekee itatoka nje ya nchi kuzifuata timu za Tunisia na Angola ili tuone kama wataweza kuwafikia Yanga au laah.