Yanga kujinasua mkiani leo?
Wawakilishi wa nchi katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, Yanga SC, leo wanakwenda kutupa karata yao muhimu katika mchezo wa tatu wa Makundi dhidi ya TP Mazembe baada ya kupoteza michezo miwili ya kwanza.
Yanga leo anahitaji ushindi kwa namna yoyote ili walau kuanza kupata mwanga wa kuamka kuelekea kwenye kufuzu kwenda Robo Fainali endapo watazichanga vizuri karata zao katika michezo mingine mitatu itakayokuwa imesalia.
Msimamo kwenye kundi A la Yanga upo hivi:
Al-Hilal - alama 6
MC Alger - alama 4
TP Mazembe - alama 1
Yanga alama - 0