Wanachama TEFA hawamtaki mwenyekiti wao

Wanachama wa chama cha soka wilaya Temeke (TEFA) wamemjia juu makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho la soka nchini, TFF Athuman Nyamlani na kumtaka aachane na tabia ya kuwagombanisha viongozi wa vilabu vya soka wilayani humo.

Wakizungumza kwa pamoja, wajumbe hao kwenye kipindi cha michezo cha Sports Arena na Wasafi FM, wamesema Nyamlani anashinikiza mtu wake Ali Musa Kamtande awe mwenyekiti wa TEFA wakati wao hawamtaki.

"Kamtande hatumtaki, lakini Nywmlani kwa kutumia kofia yake ya umakamu wa Rais wa TFF anawashinikiza awe mwenyekiti wa TEFA wakati sisi hatumtaki, mgogoro wa TEFA unasababishwa na Nyamlani" walisema wajumbe hao kwa ujumla.

Nyamlani aliwahi kuwa mwenyekiti wa TEFA kabla ya kuwania umakamu wa Rais wa kwanza wa TFF, wajumbe hao pia hawaitaki katiba mpya ya chama hicho wakidai haifai

Athuman Nyamlani (kulia)





Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA