Timu ya Tabora United jioni ya leo imeichapa Azam FC mabao 2-1 mchezo wa Ligi Kuu bara katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mabao yote ya Tabora United leo yamefungwa na mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Heritier Ma Olongi Makambo moja kila kipindi akimtungua kipa namba moja wa timu ya taifa ya Sudan, Mohamed Mustafa kwa kichwa dakika ya 37 na kwa shuti la mguu wa kushoto 68.