Singida Black Stars yamtema kipa wa Sierra Leone
Taarifa kutoka Singida Black Stars zinasema kuwa klabu hiyo imesitisha mkataba wa golikipa Mohamed Nbalie Kamara ambaye pia ni golikipa wa timu ya taifa ya Sierra Leone.
Golikipa huyo amekuwa akisugua benchi huku langoni akisimama golikipa mzawa Metacha Mnata aliye katika kiwango bora sana tangu msimu uanze.