Simba ni nzuri kuliko Yanga- Ahmed Ally
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema timu yao ni nzuri kuliko ypyote katika ukanda huu wa Afrika mashariki, ina maana Simba ni nzuri kuliko Yanga.
"Timu yetu ni bora kuliko timu nyingine yoyote kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, timu yetu imeimarika sana
Mwanasimba inabidi ujivunie timu yako maana ubora wa kikosi unaongezeka siku hadi siku
Mchezo wa Jumapili lazima kila Mwanasimba ajue umuhimu wake maana mpinzani tunayekutana nae anataka kufufukia kwetu na sisi hatuko tayari kuona CS Sfaxien anafufukia kwetu
Hakuna ambaye amewahi kupata uhai ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa."
Semaji Ahmed Ally