Ronaldo kucheza kombe la dunia la 2030
Nyota wa zamani wa Manchester United na taifa la Ureno Luis Nani amesema Cristiano Ronaldo anaweza kucheza kombe la Dunia 2030 ambalo litaandaliwa na Ureno sambamba na Uhispania na Morocco ikiwa tu atazingatia mlo maalum
Ronaldo mwenye umri wa miaka 39 ataiwakilisha Selecao katika Kombe la Dunia la 2026 akiwa na miaka 41 lakini bado hajaweka wazi kuhusu kombe la dunia la 2030 ambapo atakuwa amefikisha miaka 45 licha ya mara kadhaa kukanusha malengo ya kustaafu soka hivi karibuni
“Ronaldo anajituma sana na ananidhamu ya soka unaweza kuona umri umeenda lakini bado anafunga kila siku” Nani