Pamba Jiji yaibana JKT Tanzania
WENYEJI, JKT Tanzania wamelazimishwa sare ya bila mabao na Pamba Jiji ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni leo Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Hii ni dalili nzuri kwa Pamba Jiji inayonolewa na Fred Minziro ambaye tangu alipoichukua timu hiyo imekuwa na mwenendo mzuri.