Micky Harvey Ossété kumrithi Aucho Yanga
Anaitwa Micky Harvey Ossété,Raia wa Congo-Brazzavile
huyu ni kiungo Mkabaji tegemezi katika kikosi cha Saint Eloi Lupopo ya Kinshasa Congo.
Huyu mwamba anakaba mpaka Mawimbi ya sauti za Mashabiki,
anajua pia kufunga na kuanziasha Mashambulizi,ndiyo kiungo Shoka pale Congo Brazzaville.
Katika michuano yote ya kimataifa yaliyohusisha timu za Taifa kwa asilimia zaidi ya 85 ametumikakatika kikosi cha timu ya Taifa ya Congo Brazzaville ,pia Saint Eloi Lupopo imemtumia sana katika kusaka tiketi ya kufuzu hatua za Makundi CAF Confederation Cup ✨
Hata hivyo vilabu kadhaa Africa kusini vipo kwenye vita Kali kupata Saini yake
ikiwa Yanga Watampata huyu mwamba basi tatizo la Mawasiliano na miundombinu uwanjani basi litakuwa limetibika
Ossété yupo tayari kujiunga na Yanga ,japo kwa upande yanga bado halijawekwa wazi.
Kama uhamisho wake ukikamilika basi defensive Midfielders watakuwa hawa.
1.Kelvin Nashon
2.Khalid Aucho
3.Micky Harvey Ossété
4.jonas mkude
5.Aziz Andambwile