Malengo yetu ni kufika robo fainali- Fadlu
Kocha mkuu wa Simba SC Fadlu Davids amesema malengo yao kama timu ni kufuzu hatua ya robo fainali kama vinara wa kundi A kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani afrika msimu huu 2024-25.
“Kundi bado lipo wazi tunapaswa kupambana kuiwania nafasi ya kwanza kwenye kundi. Kufuzu robo fainali ndio lengo namba moja, lakini kama ukifuzu kama kinara wa kundi utakuwa na faida hatua ya robo fainali.’’ - Fadlu Davis kocha Simba SC
Simba inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi A ikiwa na alama 3 katika michezo miwili waliyocheza mpaka sasa. Wameshinda mchezo mmoja pia wamefungwa mchezo mmoja tofauti yao na kinara wa kundi CS Constantinois ni alama 3.