KWANINI YANGA WANAPENDA KUSAJILI WACHEZAJI WA SIMBA?

Na Prince Hoza

ISRAEL Patrick Mwenda nj miongoni mwa wachezaji wapya wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara, mchezaji huyo alisajiliwa wiki hi akitokea Singida Black Stars ya mkoani Singida.

Mwenda ana uwezo wa kucheza namba mbili au tatu na alijiunga na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea klabu ya Simba SC aliyojiunga nayo akitokea KMC.

Usajili wa Mwenda umepokelewa kwa mitizamo tofauti, huku baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo wakigawana makundi, wapo wengine wanaupongeza uongozi wa Yanga kwa kumsajili wakiamini kwamba Mwenda anaweza.

Lakini pia kuna wengine wanatilia shaka usajili wake wakisema hafai na anauwezo wa kuitumikia Yanga kwa sababu alikuwa hapati namba kwenye kikosi cha kwanza cha Simba.

Kusajiliwa kwake Yanga si sahihi kwani ana uwezo wa kuanza kwenye kikosi cha kwanza, tayari Yanga ina mabeki wa pembeni na wenye uwezo mkubwa na sidhani kama Mwenda ataweza kupata nafasi ya kucheza.

Yanga ina mabeki kama Kouassi Attoholoa Yao Jeshi na Chadrack Boka ambao wamekuwa wakianza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza, lakini pia Kibwana Shomari na Nickson Kibabage wamekuwa mbadala.

Usajili wa Mwenda umeenda kutimiza idadi ya wachezaji wanne badala ya watano waliosajiliwa na Yanga wakitokea Simba, lakini usajili huo wa wachezaji kutoka Simba, unaonekana hauna mantiki yoyote kwani wachezaji hao wamekuwa mzigo.

Mpaka sasa Yanga imewasajili wachezaji kutoka Simba, Jonas Mkude, Clatous Chama, Jean Baleke na Mwenda, lakini pia walimsajili Augustine Okrah aliyetupiwa virago vyake.

Sio siri sijui Yanga wanavutiwa na nini na wachezaji kutoka Simba, kwani inapenda kuwasajili hata kama hawana nafasi ya kucheza, hata Clatous Chama amekuwa akianzia benchi kwenye kikosi cha kwanza wakati Mkude na Bsleke wote wanasugua benchi.

Mamilioni ya shilingi yanateketea na faida yao kwenye kikosi hicho haionekani, sidhani Mwenda kama anasajiliwa Yanga kwenda kukaa benchi ama kuanza kwenye kikosi cha kwanza, lakini hilo anajua kocha kwani yeye ndiyo anapanga kikosi cha kwanza.

Bila shaka Wanayanga hawaelewi hatma ya kikosi chao na mwenendo wa viongozi wao juu ya usajili wa wachezaji kutoka Simba, sijajua kwanini viongozi wao wanamulika Msimbazi.

Desturi ya Yanga kusajili wachezaji wa Simba haikuanza leo, klabu hiyo imekuwa na taratibu ya kuwachukua wachezaji wa Simba, ukiachana na miaka ya 1970 hadi 1980, miaka ya 1990 iliwasajili wachezaji wengi kutoka Simba.

Miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na Yanga ni Zamoyoni Mogella, Hamisi Gaga na Method Mogella, lakini pia nyota wengine kama Shauri Iddi, Akida Makunda, Said Maulid "SMG" na wengineo.

Ingawa pia Simba nao wamewahi kuchukua wachezaji wa Yanga, lakini Simba wamekuwa na wivu na mchezaji anayefanya vizuri ndani ya uwanja, kwa mfano imewahi kumsajili Bernard Morrison ambaye alikuwa mchezaji kipenzi cha Yanga.

Tofauti na Yanga wamekuwa wakiwasajili wachezaji wa Simba hata kama uwezo wao umeshuka, kama ilivyo kwa Mkude, Baleke na sasa Mwenda.

Hata Chama uwezo wake unadaiwa umeshuka tofauti alivyokuwa anacheza Simba, mashabiki wa Yanga wanalalamika sajili za timu yao kwa wachezaji kutoka Simba ni kama za kukomoana, lakini sasa wao ndio wanaojikomoa kwani wachezaji hao si bora ndani ya uwanjani.

ALAMSIKI


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA