Kibu apiga mawili, Simba ikiichapa CS Faxien
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC jioni ya leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya CS Faxien ya Tunisia mchezo wa kombe la Shirikisho uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
CS Faxien walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Hazzem Haji Hassen dakika ya 03 lakini Simba walichomoa kupitiavkwa Kibu Denis dakika ya 08.
Lakini Simba waliongeza bao la pili dakika ya 98 kupitia kwa Kibu akifunga la pili na kuifanya Simba ifikishe pointi 6, timu hiyo itarudiana na Fwxien mjini Tunis, Tunisia