Israel Mwenda atambulishwa Yanga SC
Klabu ya Yanga SC imetangaza kukamilisha usajili wa beki wa pembani Israel Mwenda kutoka Singida Black Star kwa mkopo wa miezi sita wenye kipengele cha kusajiliwa moja kwa moja akifanya vizuri.
Taarifa za kusajiliwa Mwenda kwenye kikosi hicho zilianza kuvuja tangu mwanzoni mwa msimu wakati anaichezea Simba SC kabla ya kuvunja mkataba.
Mwenda aliyeibukia Aliance ya jijini Mwanza, ana uzoefu mkubwa wa kucheza mashindano ya kimataifa hivyo Yanga wamepata mtu sahihi, pia anaweza kucheza nafasi zote za prmbeni na anajua kupiga free kick.