Fountain Gate mwendo mdundo yailaza Coastal Union
Timu ya Fountain Gate jioni ya leo imeifunga Coastal Union mabao 3-2 mchezo wa Ligi Kuu bara katika uwanja wa Tanzanite mjini Manyara.
Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na Elie Mukoko dakika ya 15, William Edgar dakika ya 48 na Nickolas Gyan dakika ya 56, wakati mabao ya Coastal Union yamefungwa na Lucas Kikoti dakika ya 44 na Maabad Maulid dakika ya 80