Elie Mpanzu kuwavaa KenGold
Winga mpya wa Simba SC Elie Mpanzu Kibisawala sasa ni rasmi ataanza kutumika kwenye mechi dhidi ya KenGold itayopigwa siku ya tarehe 18 mwezi huu
Dirisha la usajili la ndani linafunguliwa tarehe 16 mwezi huu na kufungwa tarehe 15 Januari na la CAF litafunguliwa tarehe 1 mwezi Januari na kufungwa tarehe 31 Januari hivyo upande wa kombe la Shirikisho Mpanzu ataanza kutumika kuanzia mechi na CS Faxien itayochezwa nchini Tunisia