Dili la Kelvin Nashon kutua Yanga laota mbaya
KELVIN Nashon alikuwa katika hatua za mwisho za kujiunga na Yanga kwa mkopo akitokea Singida Black Stars ya Singida lakini kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye vyanzo vyangu ni kuwa dili hilo kwasasa lipo 50/50 na mbioni kuota mbawa kabisa, Yanga huenda wakajitoa dakika za mwisho kwa maana hawakamilisha uhamisho huo.
Nashon (24) awali alihitajika na Pamba ya Mwanza ambapo walikubaliana maslahi na kila kitu na akasafiri mpaka Jiji la Miamba sambamba na Straika Habibu Kyombo ambapo ulikuwa ni uhamisho wa mkopo ila Kelvin alipigiwa simu baadae kuwa Yanga wanamhitaji na akasafiri kuja Dar es Salaam na walikubaliana kila kitu kabla ya kusaini kwa mkopo.
Baada ya muda mchache Nashon kwa mujibu wa vyanzo vyangu hakuwa anapata tena ushirikiano kutoka kwa Yanga ili kumaliza dili hilo na hakupewa majibu ya moja kwa moja maana ilikuwa atambulishe kabla ya Israh Patrick, kuna uwezekano mkubwa Kiungo huyo akarejea Pamba aliporipiti awali kwa mkopo endapo Yanga hawatomrejea tena ndani ya siku mbili hizi.