Cedric Kaze kurejea Jangwani
Aliyewahi kuwa kocha wa Yanga SC Cedric Kaze raia wa Burundi anarejea ndani ya klabu hiyo.
Kaze anarejea kikosini humo kwa lengo la kuongeza nguvu kwenye benchi la Ufundi lililo chini ya Kocha Saed Ramovic,
Muda wowote kuanzia sasa kocha Kaze atawaaga wachezaji wa klabu yake ya sasa ya Kaizer Chiefs na kuanza safari ya kuja Tanzania kuanza majukumu yake mapya ndani ya waajiri wake wa zamani Young Africans.