Bodi ya Ligi yainusuru Simba kwa Tabora United

Na Ikrwm Khamees

Bodi ya Ligi (TPLB) imeiondoa mechi kati ya Simba na Tabora United iliyopangwa kuchezwa Disemba 28, 2024 sasa itapangiwa baadaye.

Pia mchezo dhidi ya Simba na Singida Big Stars ambao awali haukupangiwa tarehe sasa utachezwa Disemba 28, 2024 kwenye Uwanja wa Liti mkoani Singida.

Mchezo dhidi ya Tabora United ambao ulipangwa kuchezwa Disemba 28, 2024 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora umeondolewa na utapangiwa tarehe mpya.

Kusogezwa kwa mechi ya Simba na Tabora United ambayo sasa ni moto wa kuotea mbali baada ya kuzifunga Yanga na Azam na kuigomea Singida Black Stars, Bodi ya Ligi ni kama wameisaidia Simba kutoka kwenye kichapo kwa walina Asali hao wa Tabora.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA