Baleke atemwa, ahusishwa Namungo
Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga,Jean Baleke atawakosa waajiri wake kuelekea kwenye mechi ya kimataifa ya michuano ya klabu bingwa barani Africa ya CAF.
Baleke hajasafiri na kikosi cha Yanga kuelekea mchezo wa klabu bingwa barani Africa ambapo Yanga SC watacheza na TP Mazembe ya nchini DR Congo.
Wakati huo huo mshambuliaji huyo anahusishwa kujiunga na timu ya Namungo FC ya Ruangwa na tayari wameanza mazungumzo kabla ya kusajiliwa katika dirisha hili dogo la Januari