Yanga yatosa ndoano kwa Lawi
Imesalia takribani mwezi mmoja kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa Desemba 15 mwaka huu, Yanga SC imerusha ndoano kuwania saini ya beki wa kati wa Coastal Union, Lameck Lawi ambaye awali alikuwa kwenye rada za Simba kabla ya mvutano kutokea na kila mmoja kwenda na njia yake.
Uamuzi huo wa Yanga ambao inaelezwa uko kwenye hatua nzuri za awali, umekuja baada ya changamoto walizozipata kwenye safu ya ulinzi kutokana na upungufu wa mabeki wa kati walipocheza mechi ya ligi dhidi ya Tabora United, ambapo walilazimika kuwatumia viungo Khalid Aucho na Aziz Andabwile.