Ramovic kuanza na kasi ya ajabu Yanga
Kocha mpya wa Yanga SC, Mjerumani Sead Ramovic, ameanza kwa kasi tangu alivyoteuliwa, mara baada ya kutangazwa rasmi, kocha huyo alifanya kikao cha haraka na wasaidizi wake, akiwa na lengo la kuanza kazi kwa kuangalia hali halisi ya timu. Ramovic, ambaye amekuja kwa dhamira ya kuleta mafanikio, ameonesha ari kubwa ya kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
"Kocha wetu baada ya kutangazwa hapo jana aliita kikao na wasaidizi wake, Mjerumani huyu hana kupoa kafika tu kataka kujua kila kinachoendelea na leo hii atakuwa na kikao kingine kwaajili ya kuhakikisha tunakwenda sawa kwenye maandalizi ya timu yetu kuelekea mchezo wetu dhidi ya Al Hilal tarehe 26.11.2024," amesema Ali Kamwe.
Mashabiki wa Yanga SC wanatarajia kuona timu yao ikifanya vizuri chini ya uongozi wa kocha huyu mpya, ambaye ameonyesha dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko chanya kwenye kikosi hicho.