Mwakinyo atetea mkanda, alamba milioni 10 ya mama
Bondia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo amefanikiwa kuutetea kwa mara ya pili mfululizo ubingwa wake wa WBO Africa Middleweight kufuatia ushindi wa TKO raundi ya tisa (9) dhidi ya Daniel Lartey wa Ghana katika pambano lilochezwa usiku wa kuamkia Jumapili katika ukumbi wa Were House Masaki Dar es Salaam.
Kufuatia ushindi huo, Mwakinyo amemwaga machozi kutokana na kile alichosema ni Chuki za wazi kwa watu waliotakiwa kumsaidia kwenye mchezo wa Ngumi.
Hata hivyo Mwakinyo amekabidhiwa Shilingi Milioni 10 ikiwa ni hamasa ya KO ya Mama.