Mtoto wa Samuel Eto'o atupia, Rayo Vallecano ikishinda 5-0
Mshambuliaji wa Rayo Vallecano Ettiene Eto’o (22) ambaye ni Mtoto wa staa wa zamani wa FC Barcelona Samuel Eto’o jana amecheza kwa dakika 15 akitokea benchi katika mchezo wa Copa de Rey dhidi ya CD Villamuriel.
Mchezo huo umemalizika kwa Rayo Vallecano kushinda 5-0 lakini Ettiene Eto’o akifunga dakika ya 88 ikiwa ndio goli lake la kwanza akiwa na timu hiyo.