Msuva aipeleka Stars Morocco

Bao la mshambuliaji Simon Msuva jioni ya leo limeipeleka AFCON timu ya taifa, Taifa Stars baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Guinea katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Stars imefuzu fainali hizo zitakazofanyika mwakani nchini Morocco, imefanikiwa kumaliza kundi H ikiwa na pointi 10 ikishika nafasi ya pili nyuma ya DR Congo.

Katika mchezo huo Taifa Stars inayonolewa na Hemed Moloko, imecheza vizuri mbele ya Watanzania na kuibuka na ushindi huo.

Baada ya mchezo huo na Stars kukata tiketi ya kushiriki fainali hizo, Rais wa Jsmhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewaahidi kuwapa shilingi milioni 700 kwa kufanikiwa kufuzu fainali hizo.

Hongera sana Taifa Stars

Simon Msuva akijiandaa kufunga
Msuva akishangilia bao lake
Msuva na wenzake wakishangilia


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA