Kilichomuondoa Aisha Mnunka Simba iki hapa!


Najuwa kila Mmoja anaongea lake Uongozi wa Simba Queens uliongea lakini mimi niliamuwa kukaa kimya kwa sababu mimi sipendi kuongea ongea

Sababu zipo nyingi lakini kubwa zaidi ni ile ambayo kuna kiongozi aliwaambia Wachezaji wa Simba Queens wasinipe pasi za kufunga ili nisivunje rekodi za Mshambuliaji aliyekuwa Mfungaji bora nilijisikia vibaya lakini nilipambana na nikafanikiwa kuwa Mfungaji bora pamoja na MVP wa Ligi kuu

ULIITWA KWENYE KAMATI YA NIDHAMU TFF

Hapana sijawahi kuitwa kwenye kamati ya maadili na Nidhamu ya Wachezaji lakini mimi nimepanga kwenda kwenye hiyo Kamati ili niweze kuondoka Simba Queens

UNAWADAI SIMBA QUEENS

Hapana Kiukweli Simba Queens siwadai hata mia wameshanipa haki yangu yote ambayo niliyokuwa nawadai

UNAMKATABA WA MUDA GANI NA SIMBA QUEENS

Mkataba ambao umebaki Simba Queens ni wa Mwaka Mmoja hivyo Mkataba wangu utaisha Mwishoni mwa Msimu huu

HUJUTII KUPOTEZA NAFASI YA KUCHEZA CAF CHAMPION LEAGUE

Hapana Sijutii kupoteza nafasi ya kucheza Cecafa na hiyo Caf Women Champions league kwa sababu nilishacheza Lakini pia mimi nimecheza Kombe la Dunia kwahiyo kwangu hakikuwa kitu kikubwa kuliko kucheza Caf Women Champions League

UMEJIFUNZA NINI KWENYE HILI SAKATA

Nimejifunza vitu vingi sana na ndo maana nikaamuwa kukaa kimya najuwa muda utafika na kila kitu kitakuwa sawa mimi nataka kucheza Mpira na siyo kuongea ongea

KWANINI ULIAMUWA KUBADILISHA NAMBA YA SIMU

Hahahahaha hapana sijabadilisha namba ya Simu mimi nina Simu mbili kubwa na ndogo unasemaji sipatikani na sipatikani kwa sababu ni nani ambaye anayenipigia Mimi napatikana watu wanaongea sana

UONGOZI WA SIMBA ULIKUTAFUTA

Niliongea na kiongozi mmoja wa Simba na nikamwambia kuwa siwezi kurudi kucheza Simba Queens baada ya hapo sijaongea nao tena mpaka leo hii

MALENGO YAKO KAMA MCHEZAJI NI YAPI

Kwasasa Kuna mambo nayaweka sawa nikiyamaliza nitajuwa nini nitafanya kwa sasa naendelea na Mazoezi yangu ili kujiweka sawa ila naamini muda si mrefu nitarudi tena Uwanjani


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA