Bernard Morrison alia na ubaguzi Ghana

Baada ya Ghana kushindwa kufuzu michuano ya AFCON 2025 na kupoteza mchezo wakiwa Uwanja wa Nyumbani dhidi ya Niger kwa magoli 2-1 kisha kumaliza nafasi ya mwisho katika kundi F, Nyota wa zamani wa Yanga SC na Simba SC.

Bernard Morrison kupitia mtandao wa X amesema ili mchezaji upate nafasi ya kucheza kwenye timu ya Taifa ya Ghana ni lazima uwe na mtu ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Ghana ambaye atakutengenezea mazingira ya kulitumikia Taifa hilo pasipo kujalisha uwezo wa mchezaji.

“Nilikuwa shabiki mkubwa wa timu yetu ya taifa tangu zamani hadi 2017. Niliacha hata kutazama mechi za Ghana kuanzia 2018 nilipogundua "SINA NAFASI TENA KWENYE KIKOSI HICHO".

Wanaita wachezaji wa vilabu vya daraja la pili na la tatu barani Ulaya kuwakilisha Ghana, vilabu vyao haviwezi hata kushinda michezo ya awali ya CAF Champions league, Lakini sisi tunaowakilisha nchi nje kwenye vilabu vikubwa na kushinda mataji ya ligi hatuwezi kuonekana kwa sababu hamna mtu kwenye shirikisho wa kukupigania”- Bernard Morrison


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA