Anguko la Yanga limetimia, yachapwa 1-0 na Azam

Hatimaye kwa mara ya kwanza Yanga SC imepoteza mchezo wake wa kwanza baada ya kulala kwa bao 1-0 dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Azam Complex Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, mchezo wa Ligi Kuu bara.

Hata hivyo beki wa Yanga Ibrahim Baka amepewa alioneshwa kadi nyekundu kabla ya kufungwa, na huenda kadi hiyo imewagharimu.

Goli pekee la Azam FC limefungwa na Jiblil Sillah dakika ya 34, kwa matokeo hayo Azam FC imefikisha pointi 21 na michezo 10 lakini itaendelea kubaki nafasi ya 4, wakati Yanga nayo imebakia na pointi zake 24.

Singida Black Stars inatarajia kuumana na Coastal Union usiku huu uwanja wa New Amaan Stadium Zanzibar.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA