Samatta awajaza matumaini Watanzania kufuzu AFCON

Nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta baada ya mchezo dhidi ya DR Congo waliopoteza 2-0 uwanja wa Taifa ameonyesha kuwa bado ana matumaini na timu ya Taifa.

" Ipo siku vijana watakuwa bora na kutupa furaha wa-Tanzania."

- Mbwana Samatta.

Nyota huyo licha ya kuumia kwenye mchezo huo lakini hakujali aliendelea kuipigania bendera ya nchi kwa moyo na jasho lake lote.

Stars imesaliwa na michezo miwili kwenye kampeni ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Guinea na dhidi ya Ethiopia.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI