Nyota wa Simba SC ataka lawama zote Taifa Stars apewe kocha na si wachezaji

Mchezaji wa zamani wa Simba SC na kocha wa Friends Rangers Said Msasu amewataka wapenzi na mashabiki wa soka nchini kutowalaumu wachezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars kutokana na kipigo cha mabao 2-0 toka kwa DR Congo na isipokuwa lawama zote zipelekwe kwa benchi la ufundi la timu hiyo.

"Wadau naomba nitoe maoni yangu mpira ni mchezo wa wazi makosa yake yanajirudia Tanzania tumepoteza nyumbani dhidi ya DR Congo naomba Watanzania tusilaumu wachezaji hasa kapteni Mbwana Samatta na Ally Salim".

"Sio sahihi wakulaumiwa ni benchi la ufundi walitakiwa liwe na game plan kila mechi ina uchezaji wake away na home na aina ya wachezaji na line up na sub haiwezekani tunatafuta goli inafanyika sub ya kutoa", alilalamika Msasu.

Said Msasu, mchezaji wa zamani wa Simba SC


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI