Mume wa Zari amchakaza kwa masumbwi JK

Mume wa Zari Hassan, Shakib Chams ameshinda pambano lake la ndondi dhidi ya mwanahabari maarufu wa Uganda JK Kazoora Jumamosi usiku.

Shakib hata hivyo alishinda baada ya Kazoora kujisalimisha na kumfanya mshindi wa mechi hiyo na kuzawadiwa kiasi pesa za Uganda Milion 10.

Baadhi ya mashabiki wanakisia kuwa huenda matokeo ya mechi hiyo yalipangwa, Hafla hiyo ilijaa mashabiki na watu mashuhuri miongoni mwao akiwamo Zari Hassan ambaye alienda kumuunga mkono mumewe.

Kumbuka kuwa miezi michache nyuma Mwimbaji @harmonize_tz alionyesha DM kutoka kwa Shakib ambaye alimtaka mwimbaji huyo kuingia naye kwenye ulingo kama njia ya kutafuta pesa.

Harmonize alishiriki Meseji hizo na ujumbe kwa Zari kuwa "Zari unafahamu hili? Mtu wako anajaribu kucheza na kifo," alisema


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI