Mohamed Salah agomea uwanja wa nyasi bandia

MSHAMBULIAJI wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah ameripotiwa kurejea England kwa kuwa hatocheza mchezo wa kesho dhidi ya Mauritania kwa sababu uwanja unaotumika umetengenezwa kwa nyasi bandia.
.
Taarifa ya FA ya Misri ilisema: “Benchi la ufundi likiongozwa na meneja Hossam Hassan walifanya mazungumzo na Mohamed Salah na wakaafikia kumpumzisha kwenye mechi ijayo sababu hali ya kiwanja na uchezaji wa Mauritania vinaweza kumsababishia majeraha.”
.
Mchezo huo wa kesho unatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Cheikha Ould Boidiya wenye uwezo wa kuingiza watu 8,200 ambao unapatikana jijini Nouak-chott.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI