MECHI YA SIMBA NA YANGA JMOSI ITAKUWA HIVI!

NA PRINCE HOZA

WATANI wa jadi Simba SC na Yanga SC Jumamosi ijayo watashuka dimbani katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, mchexo wa Logi Kuu bara.

Huu ni mchezo wa pili tangu zilizokitana mwanzoni mwa msimu kuwania Ngao ya Jamii, katika mchezo huo Yanga SC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Maxi Nzengeli katika dakika ya 6 kipindi cha kwanza.

Kwenye mchezo huo, Simba SC itakuwa mwenyeji huo hivyo ina matumaini makubwa ya kuondoka na ushindi, lakini rekodi za watani hao, walikutana msimu jana ambapo Yanga SC iliibuka mshindi katika mechi zote mbili.

Mzunguko wa kwanza Yanga SC iliibuka na ushindi wa mabao 5-1, huku Simba ikiwa mwenyeji, na kwenye mchezo wa marudiano Yanga tena iliibuka mshindi kwa mabao 2-1.

SIMBA NA MATUMAINI MAKUBWA YA KUSHINDA

Simba SC inayonolewa na Fadlu David's raia wa Afrika Kusini, ina matumaini makubwa ya kupata ushindi kwenye mchezo huo, matumaini ya Wanasimha yanatoka kwa wachezaji wao iliyowasajili mwanzoni mwa msimu huu.

Lakini matumaini mengine yanakuja kutokana na rekodi za timu hizo mbili kwamba haiwezekani kwa timu moja kumfunga mwenzake mara nne mfululizo, hapo awali ilikuwa haijatokea kwa timu moja kumfunga mwenzake mara tatu mfululizo.

Lakini zilipokutana kwenye Ngao ya Jamii, Yanga ikawafunga Simba msra tatu mfululizo huku kocha wa Yanga, Miguel Gamondi raia wa Argentina kuweka rekodi, matumaini mengine ambayo Wanasimha wanajivunia nayo na mabadiliko ya kikosi chao, kwa vyovyote Simba wanajiamini kupata ushindi.

Mashsbiki wa Simba wanavyoamini kwamba Yanga haitishi kwa lolote hivyo wanaenda kuipa kipigo, kwa kifupi kuna wengine wanaamini mambo ya ushirikina kwamba Simba wamejipanga sana kupata ushindi, ingawa mimi siamini.

YANGA WANA JAMBO LAO

Kuelekea mchezo huo wa watani wa jadi, Yanga wataingia uwanjani kama mgeni, lakini hata hawaihofii Simba na wanajipa matumaini ya kushinda kama ilivyo kawaida yao.

Yanga wao hawaamini masuala ya timu moja haiwezekani kumfunga mwenzake mara nne, wao wanatambia kikosi chao na kwenye mchezo huo wataingia uwanjani kwa lengo la kupata ushindi mwingine ikiwa ni wa mara nne mfululizo.

Yanga wanaamini wanakikosi bora na huenda isije kutokea tena kuwa bora kama ilivyo sasa, hivyo ni wakati wao kushinda mbele ya Simba, kwa kifupi mechi za watani ikikaribia mioyo ya watu inaenda kasi, na ndio maana kuna watu wanazimia siku ya mchezo na wengine hupoteza maisha.

ZILIVYOSASA

Simba kwasasa ina pointi 13 ikiwa imecheza mechi 5, wakati Yanga Ina pointi 12 ikiwa imecheza mechi 4, mechi za mwisho kabla hazijakutana Jumamosi, Simba walianza kucheza na Coastal Union ya Tanga katika uwanja wa KMC Complex, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Simba na Coastal zilitoka sare kwa kufungana mabao 2-2, wakati Yanga ilicheza na Pamba Jiji FC ya Mwanza, katika mchezo huo Yanga ilishinda mabao 4-0 kwenye uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Kwa kifupi dabi haina mwenyewe ila Yanga itaendelea kuwa juu ya Simba na mimi nawapa asilimia 65 wakati Simba nawapa 35, kikubwa tumuombe mwenyezi Mungu atupe uhai na afya njema ili kusudi tushuhudie mtanange huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na wengi.

ALAMSIKI








Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI