Edo Kumwende aipa nafasi Yanga kwa MC Alger


Yanga dhidi ya MC Alger? Inanikumbusha mechi ya Yanga na Club Africain. Inanikumbusha pia mechi za Simba na Wydad Casablanca.

Yanga ilishinda kwa Waarabu kwa bao la Aziz Ki katika mechi ambayo iliupiga mpira mwingi. Lakini tazama mechi za Simba na Wydad. Kuanzia Temeke hadi Casablanca hazikuwa ngumu.
.
Waarabu wana mashabiki wanaotisha lakini kwa sasa wana timu za kawaida tu. Bingwa wao aliyepita kabla ya huyu USM Alger alipata wakati mgumu kwa Yanga katika mechi zote mbili.
.
Fainali ya kwanza Yanga walijichanganya Dar es salaam wakachapwa 2-1. Fainali ya pili wakashinda moja bila pale Algiers.

Sioni kama Yanga wanatishwa na timu za Afrika Kaskazini kwa sasa. Yanga hii ya akina Pacome ni ya moto. Ina wachezaji wengi wenye maarifa mengi.”


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI