Duchu alikubali benchi

Beki wa kulia wa Simba David Kameta ‘Duchu’ amesema kama mchezaji anatamani kucheza lakini mchezaji anaepata nafasi ya kucheza mara kwa mara Shomari Kapombe anatekeleza vizuri majukumu kwenye eneo lake ndio maana anaendelea kucheza mara kwa mara.

Duchu ameongeza kuwa bado hajakata tamaa, anaamini ipo siku ataaminiwa na kupewa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Eneo la ulinzi wa kulia la Simba lina wachezaji watatu, Shomari Kapombe, David Kamera ‘Duchu’ na Kelvin Kijili lakini hadi sasa bado chaguo la Kocha wa timu hiyo Fadlu Davids kimekuwa kwa mkongwe Kapombe na mara kadhaa Kijili amepata nafasi kwenye kikosi cha Simba.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI