Yanga na Chama kimeeleweka

Klabu ya Yanga SC imefikia makubaliano na kiungo wa kimataifa wa Zambia na klabu ya SimbaSC, Clatous Chama ya kumsajili kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mmoja zaidi iwapo atafanya vizuri ndani ya miezi sita (6) ya mkataba wake.

Chama mwenye umri wa miaka 32 atapewa dola 150,000 (zaidi ya milioni 380 za Kitanzania) kama ada ya usajili na mshahara wa dola 13,000 (zaidi ya milioni 33 za Kitanzania) kwa mwezi. Pia ameahidiwa kupewa dola 150,000 akiongeza mkataba wa mwaka mmoja.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI