Timu ya Job yaichakaza timu ya Kibwana 5-2, Hersi, Dube watupia

Timu ya beki wa kati wa Yanga SC Dickson Job jioni ya leo imeichakaza timu ya beki wa pembeni wa Yanga pia katika mchezo wa kirafiki uliopewa jina la Wape Tabasamu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Licha kwamba mpira ulikuwa mzuri na wa kupendeza, timu Job ilikuwa ya kwanza kuandika bao kupitia kwa Hersi Said dakika ya 13 kabla ya Said Ndemla dakika ya 23 kuongeza  la pili.

Prince Dube dakika ya 26 aliandika bao la tatu, lakini Simon Msuva dakika ya 30 na 47 aliifungia mabao mawili timu ya Kibwana Shomari, George Mpole dakika ya 70 alifunga bao la nne na Samson Mbangula aliweka bao la tano dakika 79 na Edwin Balua dakika ya 90 alihitimisha kalamu ya mabao


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI