Simba, Yanga na Azam msituletea utoto wa kuwapa thank you wachezaji wanaoachwa

Na Prince Hoza

ALIANZA kupewa thank you nahodha John Raphael Bocco maarufu Adebayor akafuatia Said Ntibanzokiza au Saido kama anavyojulikana, thank you ziliendelea kwa Shabani Chilunda na Luis Miquissone.

Na bado klabu ya Simba kila kukicha inawapa thank you wachezaji wake inaowaacha, kwa maana wapenzi na mashabiki wa soka wa klanu hiyo na wote kwa ujumla wanatakiwa kuwasha data simu zao au kompyuta ili kujua nani anapewa thank you.

Huu ni mtindo mpya wa kuwaacha wachezaji ulioanza msimu uliopita ambapo timu ilitaka kuwatema wachezaji wake hutangaza thank you yaani inaachana na mchezaji husika.

Kuanzia Simba, Yanga na Azam walianza na staili hiyo ya thank you, kuna baadhi ya mashabiki wa soka wametokea kufurahishwa na staili hiyo ya kuwapa thank you wachezaji wake ilioshindwana naye.

Lakini kuna mashabiki wengine hawafurahishwi hata kidogo na staili hiyo, ila najua kwamba Simba, Yanga na Azam zinafanya biashara kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii.

Kitendo cha mashabiki wake kununua vocha na kujiunga mbs na kuwasha data ambapo klabu inapata gawio toka kwenye wamiliki wa mitandao kwa mfano Istagram, YouTube, Tik Tok, Blogs na nyinginezo

Kuna ajira mpya zimezaliwa kutoka na uandishi wa namna hii ya kupost thank you za timu kama Simba, Yanga na Azam.

Kwakifupi mimi binafsi sifurahishwi na thank you ya Simba, Yanga na Azam, jana nimeona thank you ya timu ya Asante Kotoko ya Ghana, kilichonifurahisha kwa Asante Kotoko ni kitendo cha kuwaacha wachezaji wake saba kwa mfululizo

Inakuwaje Simba wanatoa thank you kwa mchezaji mmoja au wawili kila siku, waelewe fika kwamba muda hautoshi, watu wanataka mchezaji mpya, hata kama itatambulisha m mchezaji mmoja sio mbaya kwani ujio wa mchezaji mpya ni tofauti na wa zamani.

Simba inatuletea utoto, ifahamike wazi kwamba kutangaza kuacha wachezaji saba au nane kwa klabu ya Simba kutawapunguzia muda wa kufuatilia habari za wachezaji wanaogtemwa ambao hawana umuhimu wowote na timu husika.

Najua hizi ni biashara za watu, lakimi wanaofanya hivyo wanatulelea utoto, nilitegemea Simba ingewapa thank you wachezaji wake walioprmdekezqa na kocha, hichi kinachofanyika cha kuwapa thank you mchezaji mmoja kinaboa wengi.

Ingependeza sana klabu kama Simba ijikite kwenye biashara za mitandao kwa kuanika wachezaji wake wapya ambao watauza jezi za msimu ambapo mwisho wa siku itangaze kama imeuza kiasi gani za jezi.

Biashara ya mtandaoni ya thank you ya wachezaji wote ingependeza sana lakini ya mchezaji mmoja haifai na inaboa, nitashangaa sana kama Yanga na Azam nazo zikaja na staili kama hii ya kuwapa thank you mchezaji mmoja mmoja.

Mwisho tuangalie ya kufanya na sio thank you ya mchezaji mmoja mmoja, Wafanzania tusionekane kama hatuna shughuri za kufanya na badala yake kuwekana bize kwa kuona mchezaji mmoja leo anapewa thank you.

ALAMSIKI


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI