Philipe Kinzumbi aitosa Yanga na kutimkia Morocco
Winga wa kimataifa wa DR Congo,Phillipe Kinzumbi amejiunga na Klabu ya Raja Casablanca kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.
Kinzumbi ilikuwa asajiliwe na Yanga SC ya Tanzania na ilisemekana kwamba Yanga itabadilishana na Kennedy Musonda lakini dili hilo limeota mbawa kwani ametimkia Morocco