Mastaa wa zamani Yanga watembelea Avic Town
Wachezaji wa zamani wa Klabu ya Young Africans Sports Club leo wamewatembelea na kuzungumza na vijana 22 wa Safari Champions, walioweka kambi AVIC Town kujiandaa na mchezo Maalum wa Safari Lager Cup, utakaopigwa Jumamosi ya June 29, 2024 katika uwanja wa Mkapa, Jijini Dar Es Salaam.
Magwiji waliotembelea kambi hiyo leo ni pamoja na Edibily Lunyamila, Kenneth Mkapa, Steven Names, Said Maulid, Omary Hussein na Salvatary Edward.