Luis Miquissone kusalia Simba

Luis Miquissone ataendelea kusalia katika klabu ya Simba SC baada ya mazungumzo ya kuvunja mkataba kushindikana.

Miquissone alirejeshwa katika klabu hiyo.akitokea Al Ahly ya Misri alikosajiliwa msimu wa 2021/2022 akitokea Simba SC akiwa kwenye kiwango bora.

Hata hivyo kiwango chake kimeshuka na sababu kubwa ikitajwa kuwa ni uzito ambapo kiungo mshambuliaji huyo kunenepeana na kumfanya ashindwe kuonyesha uwezo wake kama aliokuwa mwanzo.

Inadaiwa kwamba analipwa milioni 45 kwa mwezi, ambapo Simba inataka imtoe kwa mkopo, lakini wasimamizi wake wamekataa na pia mpango wa kuvunja mkataba nayo imeshindikana


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI