Jobe gumzo kila kona
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza kuwa baadhi ya vilabu kutoka nchi mbalimbali vimegonga hodi Msimbazi zikihitaji huduma ya mshambuliaji wa Simba Pa Omar Jobe kwenye dirisha kubwa la usajili.
Pa Omar Jobe hakubahatika kuwa na msimu mzuri kwenye timu hiyo baada ya kusajili kwenye dirisha dogo akichukua nafasi ya Moses phiri ambapo alifanikiwa kufunga goli moja ligi kuu na goli moja kwenye michuano ya Cafcl.