Ibrahim Ajibu afufua mazungumzo ya kubaki Coastal Union

Winga Ibrahim Ajibu ameanza mazungumzo mapya na Coastal Union, baada ya kumaliza mkataba wake wa mwanzo msimu ulioisha, wakati huo huo mkononi mwake akiwa na ofa za timu nyingine za Ligi Kuu.
.
Ukiachana na Coastal Union, timu nyingine zinazotajwa kumpelekea ofa Ajibu ni Namungo, KMC na Kagera Sugar na rafiki wa karibu wa mchezaji huyo, ameeleza anaangalia ni timu yenye maslahi mapana ili asaini.
.
Staa huyo wa zamani wa Simba, Yanga na Azam ni miongoni mwa wachezaji wenye uzoefu mkubwa kwenye Ligi na ndio sababu kubwa ya makocha mbalimbali kutaka kuwa nae kikosini.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI